Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A‘rafi katika hotuba za Swala ya Ijumaa ya tarehe 12 December 2025, iliyofanyika katika Muswalla Quds Qum Iran, alisema: Aya ya 35 ya Suratul-Maida inasema:
{یَا أَیُّهَا الَّذِینَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَابْتَغُوا إِلَیْهِ الْوَسِیلَةَ وَجَاهِدُوا فِی سَبِیلِهِ لَعَلَّکُمْ تُفْلِحُونَ}
Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na tafuteni njia ya kumkaribia, na piganeni jihadi katika njia Yake ili mpate kufaulu.”
Khatibu wa Ijumaa wa Qum alibainisha: Mwenyezi Mungu katika aya hii anawausia waumini juu ya taqwa, na baada ya hapo anatoa amri mbili kwa ajili ya kuitimiza vyema takwa hilo. Amri ya kwanza ni: “Wa-btaghū ilayhi al-wasīlah.”
Hapa kuna tafsiri mbili. Ya kwanza ni kwamba “wasīlah” ni jumla ya matendo yote mema; kila tendo na tabia njema ni njia ya kuifikia taqwa, na mtu anapaswa kuyaheshimu yote. Ya pili ni kuwa “wasīlah” inamaanisha Uimamu, na lazima uimamu uwe ndio njia. Njia ya kuifikia takwa ni kutembea katika mwendo wa Mtume, Imam na Walii.
Amri ya pili katika aya hiyo ni: “Wa jāhidū fī sabīlih.” Hii ina maana kwamba kufikia taqwa ya kiroho na kutembea katika njia ya Mwenyezi Mungu kunahitajia kufanya bidii. Hapa inahusisha jihadi ya ndani na ya nje, na inakusanya jihadi kubwa na ndogo.
Imam wa Ijumaa wa Qum, akielezeaa juu ya kuzaliwa kwa Bibi Zahra (a.s) na kuienzi nafasi ya mwanamke na mama, alisema: Kwa kuzingatia maelekezo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi, sisi katika mjadala wa mwanamke, familia, mwanaume tunao muundo kamili na mkamilifu ambao tunapaswa kuutangaza na kuuonesha, na kupinga kifikra na kimaudhui mantiki potofu ya Magharibi kuhusiana na jinsia, mwanamke na familia. Hili ni jukumu la Hawza, vyuo vikuu, wasomi na harakati za kiufahamu na kimapinduzi.
Akaongeza: Leo mawimbi mazito kigezo cha tatu cha mwanamke yamekifanya kuwa lengo, Sisi tunamfasiri mwanamke kwa kigezo cha Fatima, kigezo ambacho kutoka upande mmoja kiko juu katika ibada na maarifa, na kutoka upande mwingine kina nafasi ya uongozi katika kuongoza umma. Huu ndio mfano wa mwanamke wa Kiislamu: familia bora, yenye kujitolea na yenye muelekeo. Tunapaswa kujivunia kigezo hiki.
Mkurugenzi wa Hawza Iran, aliendelea: Katika muundo wa Kiislamu, maslahi jumuishi ya mwanamke, mwanaume, watoto na jamii huzingatiwa katika kuweka kanuni. Tukikusanya mizania ya maslahi haya manne, muundo wa Kiislamu hutimia. Pia ni lazima tuchukue kwa uzingativu maslahi ya sasa na ya baadaye, ya dunia na Akhera. Huenda leo matamanio yakawaita watu kwenye vurugu za kijinsia, lakini ni lazima kufikiria juu ya baadaye pia. Mantiki ya Uislamu ni ya kina na ya ujumuishi.
Imam wa Ijumaa wa Qum alikumbushia: Baadhi ya misukosuko na changamoto kubwa katika mfumo wa Magharibi kuhusu mwanamke na watoto ni matokeo ya mtazamo wa kiholela uliotokea miaka ya nyuma na uliowafikisha hapa.
Mkurugenzi wa Hawza akasisitiza: Wote tunapaswa kuwa wabebaji wa ujumbe wa maisha ya familia yenye afya na uhusiano sahihi kati ya mwanamke na mwanaume. Taasisi na viongozi lazima waamini umuhimu wa jambo hili na kulifuatilia kwa hamasa. Mawazo yoyote yenye kudhuru misingi hii kwa namna ya mpangilio lazima ishughulikiwe ipasavyo na mahusiano sahihi yahimizwe.
Khatibu wa Ijumaa wa Qum, akirejea Wiki ya Umoja wa Hawza na Chuo Kikuu, aliendelea: Umoja na muunganiko wa Hawza na Chuo Kikuu ndio unaoleta ufanisi kwa jamii, na katika hili jukumu la wasomi ni zito.
Akasema: Upuuzi wa Marekani unaendelea, Marekani na utawala wa Kizayuni kwa mara nyingine wameteketea katika tathmini zao potofu. Wanadhani kwamba mapigo waliyotoa yamerudisha nyuma harakati za muqawama au kudhoofisha azma na irada ya mataifa huru kutoka Venezuela hadi eneo hili na Iran ambayo ni moyo wa muqawama. Mmekiri faili baya na jeusi mno katika miaka ya karibuni na mmewatenda uovu binadamu na hata taifa lenu.
Mkurugenzi wa Hawza aliendelwa kusema: Iran leo iko tayari na imara zaidi kuliko zamani, na licha ya matatizo na misukosuko kama vita ya kulazimishwa ya siku 12, bado ipo tayari, msijidanganye taifa hili lipo tayari, halitasalimu amri, na litabaki imara mbele yenu.
Kuhusu taswira ya mustakabali kama njia ya kumuongoza mwanadamu
Ayatullah A‘rafi katika hotuba ya kwanza alisema: Imam Ali (a.s) katika khutba ya 82 anakumbushia juu ya kupita katika “Siraat” Siku ya Kiyama, na anatoa taswira ya safari ya mwanadamu kuanzia kifo, sakarat, barzakh, halafu matukio ya Kiyama, na hatimaye Peponi au Jahannam.
Akaendelea kusema: Mojawapo ya njia za kumuongoza na kumwamsha mwanadamu ni kumwekea taswira ya matukio yajayo. Kutazama mustakabali na kujenga picha ya safari ya milele ni njia ya kuijenga nafsi na malezi ya kiroho. Siri ya kufanikiwa kwa mwanadamu ni kutokuangaika na “leo” tu, bali pia kutazama upeo mpana wa baadaye.
Mkurugenzi wa Hawza akabainisha kuwa: Mustakabali na taswira vina nafasi muhimu sana katika ukuaji na ustawi wa mwanadamu katika nyanja zote. Miongoni mwa taswira hizo ni “daraja la siraat” Siku ya Kiyama, ambalo limeelezwa katika Qur'ani na hadithi nyingi. Daraja hili ni jepesi kuliko unywele na kali kuliko upanga, na kupita juu yake ni kazi ngumu mno kwani hupita juu ya Jahannam.
Akaongeza kuwa: Siraat ni taswira ya ugumu wa mitihani ya dunia, na kupita juu yake ni mfano wa kuvuka mitihani na matamanio ya dunia. Imam Ali (a.s) anasema:
اعلَمُوا أنَّ مَجازَکُم علی الصِّراطِ و مَزالِقِ دَحضِهِ و أهاوِیلِ زَلَلِهِ و تاراتِ أهوالِهِ
“Jueni ya kwamba njia yenu itapita juu ya Siraat, na kwenye maeneo yake ya kuteleza, na vitisho vyake, na hali zake za kutisha kwa zamu.” Kupita Siraat ni lazima kwa kila mwanadamu.
Imam wa Ijumaa wa Qum akaeleza pia: Imam Ali (a.s) anasema:
فاتَّقُوا اللّه عِبادَ اللّه تَقیَّةَ ذی لُبٍّ شَغَلَ التَّفکُّرُ قَلبَهُ وأنصَبَ الخَوفُ بَدَنَهُ
“Enyi waja wa Mwenyezi Mungu! Mcheni Mwenyezi Mungu kumcha kwa yule mwenye hekima ambaye tafakuri imetawala moyo wake na khofu [ya Mwenyezi Mungu] imedhoofisha mwili wake.”
Huu ndio upeo wa taqwa ambao Imam Ali (a.s) anauoneshaa mbele yetu.
Ayatullah A'rafi akizungumzia Nahjul-Balagha alisema: Hotuba na barua za Nahjul-Balagha zilikuwepo hata kabla ya Sayyid Radhiy, na bila shaka kitabu hiki ni mkusanyiko wa maneno ya kiungu yaliyounganishwa na hazina ya elimu ya ghaibu ya Imam Ali (a.s). Kitabu hiki ni mauzo ya maneno ya Imam Ali (a.s) kutoka hazina pana ya hotuba na barua zake, kwani maneno yake yamehesabiwa kufikia 10,000 na hotuba zake kufikia takribani 500.
Akaongeza: Wingi wa tafsiri na sharh za Nahjul-Balagha ni miongoni mwa dalili za umuhimu wa kitabu hiki. Licha ya kuwa tafsiri nyingi zimeandikwa, bado siri nyingi zimefichika ndani yake na zinahitaji sharh za kina kutokana na mitazamo tofauti.
Khatibu wa Ijumaa wa Qum akabainisha: Mvuto na kina cha maneno haya vimesababisha wanafikra wa Kishia, Kisunni na hata wasio Waislamu kufanya utafiti na kuandika sharh na tafsiri. Hasan bin Abi al-Hadid, Muhammad Abduh na Subhi Saleh ni miongoni mwa masunni waliosherehesha kitabu hiki na kwa upande wa Mashia, Qutb Rawandi, Ibn Maytham Bahrani, Maghnia na Allamah Khui waliandika sharh. Katika zama hizi pia, Allamah Hasan Zadeh Amoli, Allamah Muhammad Taqi Jafari, Allamah Shushtari, Ayatullah Makarim Shirazi na Ayatullah Jawadi Amoli pia wameandika sharh muhimu.
Maoni yako